Jumapili 24 Agosti 2025 - 00:26
Mkusanyiko mkubwa wafanyika Mumbai kwa ajili ya kuliunga mkono taifa la Palestina

Hawza / Raia wa Mumbai wakiwa pamoja na viongozi wa kisiasa, maulamaa, wanaharakati wa kijamii na wasanii, walikusanyika kwa wingi katika uwanja wa Azad wa mji huo, sambamba na kutangaza mshikamano wao na watu wa Palestina waliodhulumiwa, na pia walilaani vikali jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni

Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjuma ya Shirika la Habari la Hawza, raia wa Mumbai wakiwa pamoja na viongozi wa kisiasa, maulamaa, wanaharakati wa kijamii na wasanii, walikusanyika kwa wingi katika uwanja wa Azad wa mji huo, na sambamba na kuunga mkono watu wa Palestina waliodhulumiwa, walilaani vikali jinai zinazo fanywa na utawala wa Kizayuni, mkusanyiko huu, ambao ulipewa ruhusa na Mahakama Kuu ya Mumbai na kuandaliwa kwa ubunifu wa Chama cha Kikomunisti cha India na baadhi ya makundi ya Kiislamu, ulikuwa na mandhari yenye hamasa kubwa ya mshikamano wa umma na taifa la Palestina.

Washiriki wa mkusanyiko huu sambamba na kulaani uvamizi wa utawala wa Kizayuni na mauaji ya raia wasio na hatia huko Ghaza, waliitaka jumuiya ya kimataifa kutonyamaza mbele ya jinai hizi, bali ichukue hatua za haraka, madhubuti na zenye ufanisi ili kukomesha vizuizi na dhulma dhidi ya taifa la Palestina.

Katika hafla hii, wazungumzaji katika hotuba zao walisisitiza juu ya ulazima wa mshikamano wa kimataifa na watu wa Palestina, na uvamizi pamoja na jinai zinazofanywa na utawala wa Kizayuni waliviona kuwa ni mfano dhahiri wa ukiukaji wa haki za binadamu.

Mkusanyiko mkubwa wafanyika Mumbai kwa ajili ya kuliunga mkono taifa la Palestina

Katika sehemu ya mkusanyiko huu, Hujjatul-Islam Sayyid ‘Akif Zaidi, mmoja wa wahubiri wa India, aligusia falsafa ya kuandaa mikusanyiko kama hii kwa kusema: “Mkusanyiko huu siyo tu kwa ajili ya kuliunga mkono taifa la Palestina, bali ni utetezi wa wanyonge na waliodhulumiwa wote duniani, sisi siyo maadui wa taifa au dini yoyote, bali tunaupinga kila mfumo dhalimu, iwe dhulma hii ipo katika sura ya uvamizi wa Israel au popote pale duniani na hata katika nchi yetu wenyewe, mkusanyiko wa leo ni alama ya kuheshimu thamani za kibinadamu na misingi ya kimaadili.”

Akiendelea huku akiwashukuru waandaaji na washiriki, alisema kwamba; “uwepo mpana wa wananchi ni dalili ya mwamko na uwajibikaji,” Kisha akaongeza: “Wale ambao, licha ya kujua wazi hali ya kudhulumiwa kwa Palestina, wanapuuza suala hili, wanapaswa kujitathmini upya katika ubinadamu na dhamira zao.”

Mkusanyiko mkubwa wafanyika Mumbai kwa ajili ya kuliunga mkono taifa la Palestina

Hujjatul-Islam Sayyid ‘Akif Zaidi pia, kwa kusisitiza kwamba ushindi wa kweli wa Palestina hautapatikana kwa hisia za kimaadili na kauli za kidhahania tu, alisema: “Ukombozi wa taifa la Palestina uko mikononi mwa muqawama halali na mapambano ya haki, bila shaka siku itafika ambapo wale watawala na wanasiasa wanaozima leo sauti ya Wapalestina kwa kutumia lebo ya ugaidi, kesho wao wenyewe watajitokeza kujiita watetezi wa taifa hili.”

Mwisho alibainisha: “Msaada wenu wa leo kwa waliodhulumiwa ni hatua yenye thamani na yenye kuamua hatima, lakini safari hii bado inaendelea, bila shaka majina ya wale ambao katika njia hii wanatimiza wajibu wao wa kibinadamu na kidini, yatasajiliwa katika kurasa za kumbukumbu tukufu na za heshima za historia.”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha